Waziri Mkuu akagua maendeleo ya ujenzi uwanja wa ndege Shinyanga

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga afanye kazi usiku na mchana ili kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa uwanja huo ikiwemo ufungaji wa taa na uanze kutumika wakati wote.

Amesema kuwa uwanja huo niwa kimkakati uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu na wakazi wa mkoa wa Shinyanga na maeneo ya jirani ikiwemo mkoa wa Simiyu.Amesema hayo siku ya Jumapili (Februari 16, 2025) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga ambao kwa ujumla ujenzi wake umefikia Asilimia 73.9.

“CHICO tunajua unafanya kazi nzuri, hapa kasoro yako unachelewesha kuingiza vifaa vilivyobaki, Meneja wa TANROAD ameniambia mmekamilisha kwa asilimia 100 kwenye eneo la kuruka na kutua ndege, sio kweli, bado taa, kwahiyo agiza taa mara moja zije hapa, tunaweza kuutumia uwanja wetu usiku, hata kama jengo halijakamilika, mnaweza kutumia jengo la zamani, hamdai chochote fedha zote mmelipwa.

Amesema kuwa dhamira ya Serikali ya kuendelea kuimarisha Sekta ya usafirishaji ni dhamira kamili na kwasasa inatekelezwa kwa vitendo “Leo hii kila mkoa tuna uwanja wa ndege ukiondoa mikoa mipya ikiwemo Simiyu lakini Serikali inaendelea na ujenzi katika maeneo hayo.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka Watanzania waliofanya kazi za ujenzi kwenye uwanja wa ndege wa Shinyanga kutumia uzoefu na ujuzi walioupata kujiendeleza na ikiwezekana kuanzisha makampuni ya ujenzi ili kunufaika na miradi mingine itakayotolewa na Serikali.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *