Chama Cha Mapinduzi kupitia mkutano mkuu maalum wa 2025 kiliwasilisha jina la Stephen Wasira kupigiwa kura kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Tanzania Bara.
Stephen Wasira alipendekezwa kuchukua nafasi ya Abdulrahman Kinana aliyeomba kupumzika kwenye nafasi hiyo mwishoni mwa Mwezi July 2024.
Jina la Stephen Wasira lilianza kuteuliwa na kujadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu na baadaye kufikishwa katika halmashauri kuu ya Chama kabla ya kutangazwa kwenye mkutano mkuu ambapo wajumbe walipigia kura jina hilo.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alitangaza matokeo baada ya kura za wajumbe ambazo zilimpa ushindi wa kishindo Stephen Wasira akipata kura za ndio 1910 (99.42%) kati ya kura 1917 zilizopigwa huku kura za hapana zikiwa 7.
Aidha, Stephen Wasira baada ya ushindi huo amesema kuwa jambo la kwanza atakalolifanya ni kuhakikisha CCM inaendelea kushika dola na pia ataendeleza maridhiano.