Vitambulisho vya NIDA kupatikana ndani ya siku 14.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameeleza mkakati wa Serikali ni kuhakikisha Mwananchi anapata Kitambulisho cha Taifa ndani ya siku 14 mara baada ya kukamilisha usajili katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Ameeleza hayo, tarehe 28 Februari 2025 katika hafla ya Jubilei ya miaka 25 ya huduma ya Kolping Hotel, Bukoba Kagera ambapo alitumia nafasi hiyo kueleza mikakati ya Serikali katika kuboresha utoaji wa huduma za NIDA kwa wananchi.

Mkakati uliokuwepo kwa sasa, mwananchi atakapojisajili ndani ya siku 7 atapokea namba yake ya NIDA (NIN) katika namba ya simu aliyoijaza kwenye fomu na baada ya siku 14, atapokea ujumbe mwingine wa kumtaarifu kufuata kitambulisho chake katika ofisi za NIDA amesisitiza Bashungwa

Bashungwa amewaagiza viongozi wa NIDA ngazi za Wilaya na Mikoa kutoa elimu kwa Wananchi juu ya mpango mpya wa utoaji huduma ambao umelenga kuondoa kero zote zilizokuwa zinalalamikiwa na wananchi kuhusu usajili, uzalilshaji na usambazaji wa vitambulisho hivyo.

Aidha, Bashungwa ameielekeza NIDA na Idara ya Uhamiaji kukaa pamoja katika kila ofisi za wilaya, ili kuhakikisha huduma za usajili na utambuzi zinawafikia wananchi bila usumbufu.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *