Aston Villa wamekataa ofa ya pauni milioni 60 iliyoletwa na Arsenal kumsajili mshambuliaji wake Ollie Watkins katika dirisha hili la Januari.
Zikiwa zimesalia siku 3 dirisha hilo kufungwa, Arsenal bado wanahangaika kusajili mshambuliaji wa kuziba nafasi ya Gabriel Jesus. Aston Villa wamesema kuwa Arsenal wamekuja kwa kuchelewa sana na ni ngumu kupata mchezaji atakayeziba nafasi ya Watkins muda huu.
Wakati huo huo Aston Villa wapo kwenye mazungumzo na Al Nassr kumuachia Mshambuliaji wake Jon Duran kwa ada ya pauni milioni 75.