Uwanja wa ndege Iringa mbioni kukamilika.

Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Iringa ulio katika Kata ya Nduli Mkoani Iringa umefika asilimia 93 kukamilika na inakadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 68. Uwanja huo upo tayari kwa matumizi huku safari zikitarajiwa kuanza rasmi tarehe 22 Februari, 2025 huku ndege kubwa zikitarajiwa kuwa aina ya Bombadier.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.

“Ujenzi huu wa kisasa utafungua milango ya maendeleo kwa uchumi wa Iringa pamoja na uchumi wa nchi yetu kwani utaongeza idadi ya watalii na shughuli nyingine za kiuchumi,”alisema Profesa Mbarawa.

Aidha Profesa Mbarawa ameelezea kuwa kutokana na ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya uwanja huo abiria wataweza kusafiri kwa gharama ya shilingi laki mbili na nusu (200000) hadi laki tatu (300000).

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *