Mwenyekti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Husna Sekiboko ametoa agizo kwa serikali kuhakikisha ukarabati wa uwanja wa Benjamin Mkapa unakamilika ifikapo Aprili 2025 ili kuhakikisha uwanja huo unakidhi viwango vya kimataifa kwa ajili ya mashindano ya CHAN 2024 na AFCON 2027.
Azimio hilo limetolewa wakati wa kikao cha Bunge kilichofanyika Februari 11, 2025, jijini Dodoma ambapo alisisitiza umuhimu wa serikali kuhakikisha miradi inayoendelea inatekelezwa kwa wakati ili kuleta maendeleo ya haraka kwa taifa.
Husna Sekiboko alisema “Serikali ihakikishe ukarabati wa uwanja wa Benjamin Mkapa unakamilika kwa wakati ili tuweze kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa”.
Kamati ya utendaji ya CAF iliamua kuyasogeza hadi Agosti 2024 kutokana na kutokamilika kwa maandalizi. Taarifa kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ilibainisha kuwa uamuzi huo ulichangiwa na changamoto za kiufundi na ukarabati wa viwanja