Umoja wa Ulaya (EU) kuondoa sokoni magari ya petroli ifikapo 2035

Umoja wa Ulaya (EU) una adhimia mpango wa mwaka 2035 kuondosha uzalishaji wa magari ya mfumo wa injini ya petroli kwa watengenezaji magari kumaliza mauzo ya magari mapya barani Ulaya.

Hata hivyo, nchini Uingereza, serikali ya Chama cha Labour hivi karibuni imepunguza ukomo huo adi kufikia mwaka 2030. Utengenezaji magari barani Ulaya, pamoja na malengo haya ya mazingira, kwa nadharia, unatarajiwa kutoa msingi mzuri kwa watengenezaji wa Ulaya kuongoza mabadiliko ya kimataifa kuelekea magari ya umeme. Huku ikionekana, hali si kama inavyotarajiwa.

Makampuni makubwa ya magari ya Ulaya yameshindwa mara kwa mara kushindana na wenzao wa China linapokuja suala la kuzalisha magari ya umeme yanayofikika kwa bei nafuu na yenye ufanisi. Kwa mfano, modeli kama BYD Seagull huuzwa kwa kiasi cha dola 10,000 tu nchini China, huku bei ya wastani ya gari jipya la umeme nchini Ujerumani ikiwa ni euro 52,700.

Hali ambayo imesababisha kupungua kwa mwitikio wa matumizi ya magari haya barani Ulaya.Sasa, maswali yameanza kuibuka kuhusu kama tarehe ya mwisho ya mwaka 2035 itafikiwa.

Watengenezaji magari kama BMW, VW, na Renault, pamoja na serikali ya Italia, hivi karibuni wameitaka EU kuangalia upya au kuchelewesha malengo yake.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *