Uchumi wa China wapanda kwa asilimia 5.

Uchumi wa China wapanda kwa kasi ya asilimia 5 mwaka 2024, ikiwa ni kiwango kilichokuwa chini ya mwaka uliopita huku bado kikiwa sawa na lengo la Beijing la ukuaji wa “karibu asilimia 5,” kutokana na mauzo mazuri ya nje ya mipaka na hatua za hivi karibuni zilizo chochea uchumi.

Uchumi huo uliongeza kasi katika robo ya mwisho ya mwaka, kwa mujibu wa ripoti ya serikali ya Ijumaa, ukikua kwa asilimia 5.4 kuanzia Mwezi Oktoba hadi Desemba.Mauzo ya nje yaliongezeka kwa kasi wakati kampuni na watumiaji walipokimbilia kukwepa uwezekano wa ongezeko la ushuru ambalo Rais Mteule Donald Trump angeweka kwenye bidhaa za China.

“Uchumi wa kitaifa uliendelea kuwa imara huku kukiwa na maendeleo ya hatua kwa hatua na mafanikio katika Ubora,”kwa mujibu wa ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu ilisema.

Sekta ya viwanda ilikuwa injini kubwa ya ukuaji mwaka uliopita nchini humo, huku uzalishaji wa viwanda ukiongezeka kwa asilimia 5.8 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Jumla ya mauzo ya rejareja ya bidhaa za watumiaji yaliongezeka kwa asilimia 3.5 kwa kiwango cha kila mwaka.

Mauzo ya nje yaliongezeka kwa asilimia 7.1, wakati uagizaji uliongezeka kwa asilimia 2.3.China ikiwa na uchumi wa pili kwa ukubwa duniani umekuwa ukikabiliana na matumizi hafifu ya watumiaji na shinikizo za mfumuko wa bei kutokana na kuyumba kwa uchumi baada ya janga la COVID-19 na kushuka kwa sekta ya mali isiyohamishika, ambayo hapo awali ilikuwa kichocheo kikuu cha shughuli za kibiashara.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *