Trump kuanzisha wakala wa mapato ya kodi kwa mataifa ya kigeni

Rais mteule Donald Trump Jumanne alitangaza mipango ya kuanzisha kwa wakala mpya wa Huduma ya Mapato ya Nje (External Revenue Service) kukusanya ushuru na mapato mengine kutoka kwa mataifa ya kigeni.

“Tutaanza kuwatoza wale wanaopata pesa kutoka kwetu kupitia Biashara, na wataanza kulipa,” Trump alisema Jumanne kupitia tovuti yake ya kijamii, Truth Social. Alilinganisha mpango wake wa kuanzisha wakala huo na Huduma ya Mapato ya Ndani (Internal Revenue Service), ambayo ni taasisi ya ukusanyaji wa kodi wa ndani nchini Marekani.

Kuanzishwa kwa wakala mpya kunahitaji kuhidhinishwa na Bunge,pamoja na Warepublican wanaoshikilia wingi wa viti katika Baraza la Wawakilishi na Seneti.

Trump, ambaye ameapa kupunguza ukubwa wa serikali, amekuwa akiunda wakala mpya kushughulikia kazi ambazo tayari zinashughulikiwa na mashirika yaliyopo, ikiwemo Idara ya Biashara na Forodha na Ulinzi wa Mipaka (Customs and Border Patrol), zinazokusanya ushuru na mapato kutoka mataifa mengine.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *