Trump aweka vikwazo dhidi ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu

Rais wa Marekani Donald Trump mnamo Alhamisi aliruhusu vikwazo vya kiuchumi na vya usafiri vinavyolenga watu wanaofanya kazi kwenye uchunguzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) dhidi ya raia wa Marekani au washirika wake kama Israel, akirudia hatua aliyochukua katika muhula wake wa kwanza.

Hatua hiyo inakwenda sambamba na ziara ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, mjini Washington. Netanyahu, pamoja na waziri wake wa zamani wa ulinzi na kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kipalestina, Hamas, wanatafutwa na ICC kwa madai ya uhalifu wa kivita katika Ukanda wa Gaza.

Haijafahamika ni kwa kasi gani Marekani itatangaza majina ya watu watakaowekewa vikwazo. Katika utawala wake wa kwanza mnamo 2020, Trump aliweka vikwazo kwa mwendesha mashtaka wa ICC wa wakati huo, Fatou Bensouda, na msaidizi wake wa juu kwa uchunguzi wa madai ya uhalifu wa kivita uliofanywa na wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.Vikwazo hivyo vinajumuisha kufungia mali yoyote waliyonayo nchini Marekani na kuwazuia wao na familia zao kutembelea nchi hiyo.

Mahakama ya ICC yenye wanachama 125 ni mahakama ya kudumu inayoweza kushtaki watu binafsi kwa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu, mauaji ya kimbari, na uhalifu wa uchokozi dhidi ya nchi wanachama au raia wao.

Marekani, China, Urusi, na Israel si wanachama wa ICC.Trump alisaini agizo hilo la kiutendaji baada ya maseneta wa chama cha Democratic wiki iliyopita kuzuia juhudi zinazoongozwa na Warepublican kupitisha sheria ya kuweka mfumo wa vikwazo dhidi ya mahakama hiyo ya uhalifu wa kivita.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *