Rapa Tory Lanez anayetumikia kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kukutwa na hatia kwenye kesi inayomkabili ya kumpiga risasi mguuni msanii mwenzake Megan thee Stalion amedai kuwa mwaka huu 2025 ataachiwa huru.
Tory Lanez amesema hayo kupitia Album yake mpya ya “Peterson” ambapo kwenye Outro ya Album hiyo ameidokeza dunia na mashabiki wake kuwa anaamini atakuwa huru huku akilitaja jina la Yesu na akiskika akinena kwa lugha kwenye mstari huo.
Kwa upande mwingine rapa huyo amemshukuru msanii Chris Brown kupitia album hiyo kwa kudai ndiye msanii pekee aliyemsaidia kumlipa mwanasheria wake ili amsimamie kwenye kesi yake huku akidai hakuna rapa aliyejitokeza kumsaidia katika kipindi hicho.
Album ya Tory Lanez inayoelezea maisha yake gerezani ina wiki tangu itoke na inafanya vizuri mtandaoni na kwenye mauzo ya mziki jambo ambalo limeonekana ni lakishujaa ukizingatia msanii huyo alitengeneza Album hiyo akiwa gerezani.