Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Binilith Mahenge, ameendelea na ziara yake ya kuhamasisha uwekezaji katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Katika ziara hiyo, Dkt. Mahenge ametembelea mgodi wa Mwamba na hospitali ya Waja iliyopo mkoani Geita.Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dkt. Mahenge alisisitiza dhamira ya TIC ya kuimarisha mazingira ya uwekezaji na kuwahamasisha wawekezaji wa ndani kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi.

Alisema kuwa sera za uwekezaji za Tanzania zinalenga kuleta mabadiliko makubwa kwa sekta mbalimbali za uchumi kwa kuwapa wawekezaji wa ndani nafasi za kipekee za kunufaika.”Turnefanikiwa kuwahamasisha wawekezaji wa ndani, na kwa mwaka 2024, idadi ya wawekezaji wa ndani imeongezeka ikilinganishwa na wawekezaji wa nje. Tunaendelea kuwahimiza Watanzania kwamba TIC ni chombo chao, na kuna faida nyingi wanazoweza kupata, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa baadhi ya kodi,” alisema Dkt. Mahenge.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, mkoa wa Geita umeonyesha mafanikio makubwa katika kuvutia uwekezaji. Kwa mwaka 2024 pekee, mkoa huo umesajili miradi 18 yenye thamani ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni 965. Dkt. Mahenge alibainisha kuwa TIC inalenga kusajili miradi 50 katika mkoa wa Geita ifikapo mwaka 2025, jambo linalotarajiwa kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *