Msanii maarufu wa muziki wa pop duniani, The Weeknd rasmi amebadili jina lake la usanii na sasa hataitwa tena The Weeknd badala yake atatumia jina lake halisi la Abel.
Hii ni kufikia mwisho wa safari yake ya kimuziki kama The Weeknd, kwa kufanya hivyo msanii huyo ametoa album ya mwisho kwa jina hilo kama kumbukumbu kwa mashabiki zake kwenye safari ya muziki iliyomtambulisha kama The Weeknd. Jina la album hiyo ni ‘Hurry up tomorrow’.
Msanii huyo ambaye ameachana na jina hilo amedai kuwa amekuwa akifikiria kuachana na jina hilo kutokana na presha katika kazi yake ya muziki pamoja na ushindani na kwa kuzingatia tayari ameshafanya mambo makubwa kwa jina hilo basi angetamani kufanya muziki bila presha yoyote kwa sasa.
Msanii huyo alipewa jina The Weeknd baada ya wikiendi moja kutoroka shuleni na kuamua kutorudi hali iliyofanya wenzake kumpatia hilo jina.
Licha ya kubadili jina hilo bado atalitumia kwenye mitandao ya kijamii kama utambulisho wake duniani.