Mfanyabiasha na bilionea Elon Musk amejikuta akipoteza dola billion 22.2 ndani ya siku moja na utajiri wake kwa sasa unakadiriwa kuwa dola billioni 364.3.
Mporomoki huu umetokana na kushuka kwa hisa za kampuni yake ya Tesla inayochangia nusu ya utajiri wake. Taarifa zinadai mauzo ya kampuni ya Tesla barani Ulaya yalipungua kwa takribani asilimia 50% mwezi Januari.
Athari hiyo ilipelekea hisa za Tesla kushuka kwa asilimia 8.4% na kufanya kampuni hiyo kushuka chini ya thamani ya soko la dola trilioni moja tangu Novemba mwaka jana.