Tanzania yathibitisha mtu mmoja apatikana na kirusi cha Marburg, Kagera.

Baada ya tetesi zilizoenea kuwepo kwa kirusi cha Marburg wiki kadhaa nyuma, imethibitishwa kuwa kirusi hicho kimepatikana kwa mtu mmoja tu baada ya sampuli zilizofanyiwa uchunguzi kukamilika.

Hayo yamethibitishwa na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipotembelewa na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus akiwa Ikulu ya Chamwino, Jijini Dodoma.

Aidha Rais Samia amethibitisha hakuna kifo huku akisema jitihada za wataalam zinaendelea kufuatilia kuhusu maambukizi hayo.

Maambukizi ya kirusi hicho yaliwahi kutokea hapo awali Mkoani Kagera mwaka 2023 mwezi Machi na hii inakuwa mara ya pili kutokea kwa ugonjwa huo.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *