Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ina uwezo wa kuuza umeme nje ya nchi kwa sababu mahitaji ya umeme nchini hadi kufikia mwezi Novemba mwaka 2024 yalikuwa megawati 1,888 wakati uzalishaji ulikuwa megawati 3.431.
Rais Samia ameyasema hayo leo Januari 28, 2025 alipokuwa akihutubia mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu nisharti, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) mkoani Dar es Salaam.
Aidha, ameweka bayana kuwa moja ya mipango ya Tanzania hivi sasa ni kuunganisha mtandao wa umeme uliopo nchini na nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika ili biashara ya umeme iwezeshwe kutoka Afrika Kusini hadi Misri ambapo tayari imekwishaunganishashwa miundombinu ya umeme kwa nchi za Burundi, Kenya na Rwanda huku kwa nchi za Zambia na Uganda utaratibu wa kuziunganisha ukiendelea.