Henry atupa karata yake kwa Arsenal dhidi ya Madrid.

Gwiji wa soka na mchezaji wa zamani wa Arsenal na Barcelona Thierry Henry anaamini kuwa timu yake ya zamani ya Arsenal ina uwezo wa kuitoa Real Madrid kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA) licha ya kwamba hawapewi nafasi. Henry amedai kuwa Arsenal hii inauwezo wakupambana na Real Madrid na wanachotakiwa kufanya ni […]
Newcastle bingwa Carabao.

Fainali ya kombe la Carabao imeshuhudia Newcastle United ikiibuka bingwa wa kombe hilo baada ya kuichapa Liverpool 2-1 fainali iliyofanyika katika uwanja wa Wembley. Ubingwa huo umekuwa wa kihistoria kwa Newcastle ambao wameshinda taji hilo baada ya ukame wa miaka 70 bila kombe lolote la ndani huku mara ya mwisho kubeba taji ikiwa mwaka 1959. […]
Diego Simeone alia na sheria iliyoitoa Atletico UEFA.

Kocha mkuu wa klabu ya Atlético de Madrid Diego Simeone amesema kuwa kilichofanyika kwenye mchezo wa Jana dhidi ya Real Madrid C.F. ni upuuzi tu ulifanyika. Diego Simione amenukuliwa akisema “Kwenye maisha yangu toka niwe kocha sijawahi kuona VAR inatumika kwenye mikwaju ya penalty.” “Ni sheria mpya? Imetambulishwa lini? Haman la maana zaidi ya upuuzi […]
Liverpool yatolewa UEFA.

Ligi ya mabingwa barani Ulaya imezidi kushangaza wengi baada ya klabu ya Liverpool iliyokuwa inapewa nafasi kubwa yakubeba taji hilo kujikuta inaaga mashindano hayo mbele ya Psg katika uwanja wa Anfield. Liverpool waliokuwa wanapewa nafasi kubwa yakushinda wamejikuta wanafungwa mechi hiyo iliyolazimu kuamuliwa kwa mikwaju ya penati ambapo Psg aliibuka kidedea kwa ushindi wa 4-1. […]
Zamalekh yapewa ushindi wa mezani dhidi ya Al Ahly

Masaa kadhaa baada ya Al Ahly kususia mchezo wake wa dabi dhidi ya Zamalek kwa kigezo cha kukiukwa kwa makubaliano baina ya Shirikisho la soka la Misiri na wao lakuleta marefa wa kigeni kuchezesha mchezo huo, hali imekuwa tofauti kwa Zamalek ambaye hakugomea mchezo huo na kuishia kupewa ushindi wa mezani wa alama 3 na […]
Al Ahly yagomea mchezo wa dabi.

Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri imegoma kushiriki mchezo wao wa dabi dhidi ya Zamalek kwa kile kinachodaiwa kuwa ukiukwaji wa makubaliano uliofanywa baina ya timu hizo na shirikisho la soka la Misiri (EFA). Taarifa zinadai kuwa makubaliano yalikuwa kuteua mwamuzi wa kigeni badala ya kutumia waamuzi wa ndani kwenye mchezo baina ya timu […]
Berta mkurugenzi mpya wa ufundi Arsenal.

Arsenal imemteua Andrea Berta kama Mkurugenzi mpya wa Ufundi wa klabu hiyo kuelekea msimu ujao. Berta anajiunga na Arsenal akitokea Atletico Madrid ambapo alifanya kazi kwa muda mrefu na kwa mafanikio. Katika kipindi chake Atletico Berta alifanikiwa kuwezesha usajili wa nyota kama Antoine Griezman, Luis Suarez, Julian Alvarez, Joao Felix, Angel Correa Rodrigo De Paul […]
Fainali ya kombe la dunia kuwa na onyesho kama la Supew bowl

Rais wa FIFA, Gianni Infatino amethibitisha kuwa fainali za kombe la dunia za mwaka 2026 zitakuwa na onyesho la (half time show) kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo. Onyesho hilo litafanyika tarehe 19 Julai 2026 katika uwanja wa MetLife huko New Jersey likiandaliwa kwa ushirikiano na Global Citizen huku Cold Play, Phil […]
Ligi ya mabingwa Ulaya kuendelea leo.

Raundi ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya inatarajiwa kuendelea usiku wa leo katika viwanja mbalimbali barani Ulaya. Raundi ya kwanza ya michezo hiyo inatarajiwa kuchezwa tarehe 4 na 5 pamoja na tarehe 11 na 12 ya mwezi wa 4. Timu za Arsenal, Real Madrid, Atletico Madrid, Barcelona, Bayern Munich, Liverpool na Barcelona […]
Nunez kuondoka Liverpool.

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Darwin Nunez anatarajiwa kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu ikiwa ametimiza misimu mitatu tangu alipojiunga na majogoo wa Anfield mwaka 2022. Nunez ameshindwa kufikia matarajio ya wengi tangu alipofika Liverpool akitokea Benfica, jambo ambalo limefanya Liverpool wafikirie kumuuza mshambuliaji huyo. Aidha Nunez alitarajiwa kujiunga na Al Nassr ya Saudi […]