Kauli mbiu mpya CCM “Kazi na Utu, tunasonga mbele.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, Halmashauri Kuu CCM Taifa, imefanya kikao chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo katika kikao hicho Halamshauri imepitisha kauli mbiu mpya kwaajili ya kampeni za uchaguzi wa 2025. Kauli mbiu hiyo inasema “KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE” CCM wamesema […]

ACT wazalendo wagomea vikao vya vyama vya siasa

Kamati ya uongozi taifa ya chama cha ACT wazalendo imesema haitashiriki vikao vya baraza la vyama vya siasa ikidai sababu tatu za kufikia uamuzi huo ni kutokana na vikao hivyo kugeuka jukwaa la kuhalalisha na kusafisha uchafuzi na wizi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024. Aidha wamedai kuwa baraza hilo linaloratibiwa na ofisi ya […]

Innocent Siriwa kuwania Urais Oktoba, 2025 kupitia ADC.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC) Tanzania Bara, Innocent Siriwa ametangaza nia ya kuwania Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025. Siriwa ametaja vipaumbele vitano ambayo atavipambania endapo Chama chake kitampotisha kuwania nafasi hiyo. Vipaumbele hivyo ni pamoja na elimu bure, afya bure, katiba mpya, ajira kwa vijana na Tanzania […]

Nicodemus Banduka afariki dunia.

Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Nicodemus Banduka amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80 katika hospitali ya Mloganzila Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu. Banduka anakumbukwa kama mmoja wa waasisi wa katiba ya CCM mwak 1977 inayotumika mpaka sasa vilevile amehuduma kama Mkuu wa Mkoa wa Mikoa mbalimbali ikiwemo Lindi, Pwani, Iringa, Ruvuma na Shinyanga. […]

CCM na Prosperity Party kudumisha ushirikiano na umoja.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema kuwa urafikia katia ya chama cha CCM na Prosperity Party ya nchini Ethiopia ni hatua muhimu ya kuboresha uhusiano mzuri baina ya nchi hizi mbili. Dkt Nchimbi ameyasema hayo alipokuwa akitoa salamu za CCM kwenye Mkutano mkuu wa Prosperity Party uliofanyika Addis Ababa […]

CHADEMA yateuwa Katibu Mkuu na Wajumbe wapya wa kamati kuu

Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Tundu Lissu amemteua John Mnyika kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho akiwa katika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama. Mhe. Tundu Lissu pia ameteua Manaibu Katibu Wakuu wa Chama kama ifuatavyo Wakili Ally Ibrahim Juma kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar pamoja na Aman Golugwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara. Aidha amefanya […]

Mbowe akubali ushindi wa Lissu na wenzake

Mgombe Uenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amempomgeza Tundu Lissu na wenzake kwa ushindi katika Uchaguzi uliofanyika wa kupata viongozi wapya wa Chama hicho. Licha ya kwamba matokeo bado hayajatangazwa Freeman Mbowe kupitia ukurasa wake wa X amempongeza Tundu Lissu akiashiria ndiye mshindi wa nafasi ya Uenyekiti wa Chama hicho katika uchaguzi huo huku nafasi ya […]

Dkt. Nchimbi atangazwa mgombea mwenza Urais.

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amepitishwa kugombea Urais kwenye uchaguzi wa mwaka huu kupitia Chama cha Mapinduzi amemteua Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza wake wa Urais kuelekea Uchaguzi Mkuu. Aidha Dkt. Nchimbi ataendelea kuwa Katibu Mkuu wa CCM kwa sasa hadi […]

Rais Samia kuwakilisha CCM uchaguzi 2025.

Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika Dodoma, umempitisha kwa asilimia 100 jina la Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ndiye atakayegombea Urais wa Tanzania kwenye uchaguzi wa mwaka 2025 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi. Rais Samia Suluhu Hassan alipata kura zote za ndio 1924 ikiwa ni asilimia […]

Wasira apitishwa kwa kishindo kumrithi Kinana

Chama Cha Mapinduzi kupitia mkutano mkuu maalum wa 2025 kiliwasilisha jina la Stephen Wasira kupigiwa kura kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Tanzania Bara. Stephen Wasira alipendekezwa kuchukua nafasi ya Abdulrahman Kinana aliyeomba kupumzika kwenye nafasi hiyo mwishoni mwa Mwezi July 2024. Jina la Stephen Wasira lilianza kuteuliwa na kujadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu na […]