Luambano Makamu Mwenyekiti TEFA.

Mtangazaji wa Clouds FM, Alex Luambano ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Temeke (TEFA) na Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Mohamed Saleh Mohamed. Hatua hiyo imekuja baada ya Luambano hapo awali kushindwa kwenye uchaguzi wa nafasi ya uenyekiti cha chama hicho dhidi ya Mohamed Saleh Mohamed. Kwa mujibu wa katiba ya […]
Lebron afikia rekodi ya Michael Jordan.

Katika ligi ya kikapu nchini Marekani ya NBA, nyota wa Los Angeles Lakers, Lebron James ameiongoza timu hiyo kupata ushindi dhidi ya Golden State Warriors katika ligi ya NBA. Kubwa kuliko kwenye mchezo huo ni nyota huyo kufunga pointi 42 ‘ribaundi’ 17 na Asisti 8 katika mchezo uliomfanya aungane na nguli wa mchezo huo Michael […]
Liverpool kuivaa Newcastle Wembley.

klabu ya Liverpool imefanikiwa kufuzu fainali ya kombe la Carabao baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tottenham Hotspurs katika mchezo wa nusu fainali. Mchezo huo ambao ulianza kwa Tottenham kuwa na faidi ya ushindi wa nyumbani (1-0) uliwalazimu Liverpool kutumia uwanja wao wa nyumbani vizuri kuhakikisha wanafuzu fainali hiyo. Liverpool itakipiga na Newcastle […]
Arsenal yatolewa Carabao.

Presha inazidi kupanda kwa kocha Mikel Arteta baada ya timu hiyo kutolewa kwenye michuano ya Carabao hapo jana. Mchezo huo uliokuwa na nusu fainali ulishuhudia Arsenal ikifungwa 2-0 dhidi ya Newcastle ambao waliwafunga uwanja wao wa nyumbani wiki 2 zilizopita na kufanya matokeo kuwa 4-0 kwa ujumla. Mashabiki wa timu hiyo wameanza kupoteza imani na […]
Mashabiki Arsenal wachukizwa timu yao kutosajili.

Dirisha la usajili barani Ulaya limefungwa rasmi na vilabu mbalimbali vimefanikiwa kusajili maeneo muhimu wanayohitaji ili kuweza kushindana kwenye mzunguko wa pili wa mashindano wanayoshiriki. Usajili huo umekuwa wa neema kwa baadhi ya vilabu ila umekuwa mchungu kwa klabu ya Arsenal ambayo imejikuta ikiondoka patupu kwenye dirisha hilo licha ya kuhusishwa na wachezaji mbalimbali. Mashabiki […]
Rashford kutua Aston Villa.

Klabu ya Aston Villa inatarajiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford kabla ya dirisha la usajili kufungwa siku ya Jumatatu. Marcus Rashford atajiunga na Aston Villa kwa mkopo wa wa msimu mzima huku klabu ya Aston Villa ikihusika kulipa mshahara wake. Rashford amekubali kujiunga na Aston Villa baada ya maongezi na kocha […]
Etihad pawaka moto.

Moto umezuka uwanja wa Manchester City wa Etihad masaa machache kabla ya mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Club Brugge. Moto huo umeanzia kuwaka kwenye sehemu za kuuzia Jezi hatua chache kutoka kwenye Jukwaa. Aidha taratibu kadhaa zinafanyika kuzima moto huo kabla ya mchezo huo unaotarajiwa kufanyika masaa machache siku ya leo.
Villa wapiga chini ofa ya Arsenal kwa Watkins.

Aston Villa wamekataa ofa ya pauni milioni 60 iliyoletwa na Arsenal kumsajili mshambuliaji wake Ollie Watkins katika dirisha hili la Januari. Zikiwa zimesalia siku 3 dirisha hilo kufungwa, Arsenal bado wanahangaika kusajili mshambuliaji wa kuziba nafasi ya Gabriel Jesus. Aston Villa wamesema kuwa Arsenal wamekuja kwa kuchelewa sana na ni ngumu kupata mchezaji atakayeziba nafasi […]
Hatua ya makundi UEFA Champions League kukamilika leo.

Ligi ya mabingwa barani Ulaya maarufu kama Uefa Champions League kuamuliwa leo huku zikiwa zimefuzu timu 4 mpaka sasa kuelekea hatua ya 16 bora ambazo ni Liverpool, Arsenal, Barcelona pamoja na Inter Milan. Mechi hizo za mwisho zinatarajiwa kuchezwa zote kwa wakati mmoja kuamua hatma ya timu zitazofuzu moja kwa moja kwenye hatua ya 16 […]
Michael Oliver atishiwa maisha.

Chama cha waamuzi nchini Uingereza kimesema kuwa kinasimama na maamuzi ya mwamuzi Michael Oliver baada ya sakata lake la kadi nyekundu aliyotoa ya beki wa Arsenal Myles Lewis Skelly kwenye mchezo wa Arsenal dhidi ya Wolves. Chama hicho kimesema kuwa wanaona ni kadi sahihi licha ya watu mbalimbali kupinga. Michael Oliver yupo chini ya uangalizi […]