Marcus Jordan adakwa na dawa za kulevya.

Mtoto wa aliyekuwa gwiji wa mpira wa kikapu duniani, Michael Jordan amekamatwa jijiji Florida kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa huku akikutwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine. Polisi walifanikiwa kumkamata baada ya kugundua gari lake aina ya Lamborghini limekwama kwenye reli za treni. Taarifa zinadai Marcus aligoma kushirikiana na polisi hali iliyopelekea […]

FCS na SIDO kushirikiana kuwawezesha kiuchumi makundi maalum.

Shirika la The Foundation For Civil Society FCS limetia saini makubaliano ya kushirikiana kati yake na Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) kutekeleza mradi wa miaka mitatu wa kuwawezesha kiuchumi makundi maalum ya Vijana, wanawake na watu wenye Ulemavu. Akizungumza katika hafla fupi yakutia saini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge amesema kuwa Mkataba […]

Agha Khan IV afariki dunia.

Kiongozi mkuu wa 49 wa Madhehebu ya Shia Ismailia na mwanzilishi wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), Mtukufu Aga Khan, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88 jijini Lisbon, Ureno. Mtukufu Aga Khan, anayefahamika kama Karim Al-Hussaini Aga Khan IV, alijulikana kwa mchango wake mkubwa katika kuboresha ustawi wa binadamu kupitia miradi […]

Rais Samia kuboresha maslahi ya walimu.

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itapitia upya maslahi kada ya ualimu nchini ili kuipa hadhi inayostahiki kada hiyo. Rais Samia ameyazungumza hayo Jijiji Dodoma wakati akizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2024. “Tutapitia upya maslahi ya kada ya ualimu nchini ili kuipa hadhi inayostahiki kada hii […]

Tanzania yathibitisha mtu mmoja apatikana na kirusi cha Marburg, Kagera.

Baada ya tetesi zilizoenea kuwepo kwa kirusi cha Marburg wiki kadhaa nyuma, imethibitishwa kuwa kirusi hicho kimepatikana kwa mtu mmoja tu baada ya sampuli zilizofanyiwa uchunguzi kukamilika. Hayo yamethibitishwa na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipotembelewa na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus akiwa Ikulu ya Chamwino, Jijini […]

Wizara ya Afya yathibitisha tetesi za ugonjwa wa Marburg Kagera.

Wizara ya Afya imethibitisha kupokea tetesi za uwepo wa ugonjwa wa Marburg katika Mkoa wa Kagera ambapo Wizara imepanga kutuma timu ya wataalamu kadhaa kuchukua sampuli kisha kufanyia uchunguzi Maabara. Akithibitisha tetesi hizo Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama amesema ” Mpaka Januari 15, 2025 majibu ya uchunguzi wa kimaabara kutoka kwa wahisiwa wote waliochukuliwa […]

TMA yadokeza uwepo wa Kimbunga Dikeledi

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imejulisha umma uwepo wa Kimbunga Dikeledi katika Bahari ya Hindi mwambao wa pwani ya Msumbiji. Hata hivyo kutokana na ukaribu wa maeneo ambayo Kimbunga Dikeledi kipo sambamba na maeneo ya kusini mwa nchi yetu, upo uwezekano mdogo wa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa katika maeneo ya […]

Bashungwa aomba vitambulisho vya NIDA vilivyofutwa virejeshwe

Vitambulisho 31,000 vilivyopata changamoto ya kufutika taarifa zake vimeagizwa kurejeshwa NIDA na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Innocent Bashungwa. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Innocent Bashungwa akiwa kwenye kikao kazi na jukwaa la wahariri (TEF) kilichofanyika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam amesema kuwa vitambulisho vya Taifa vilivyopata changamoto ya kufutika taarifa […]

Kikwete ashirki mkutano wa uboreshaji kilimo Afrika

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ameshiriki mkutano kuhusu uboreshaji wa kilimo barani Afrika kuelekea kupitishwa kwa programu ya kuendeleza kilimo Barani Afrika (CAADP 2026-2035) Kampala Jijini Uganda. Kikwete ameshiriki mkutano huo akiwa kama mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Chakula Afrika na mjumbe wa bodi ya Shirika la Kimataifa la Muungano […]

NMB yafungua tawi Wete, Pemba

Benki ya NMB sasa inapatikana Mikoa yote Zanzibar. Hii ni baada ya kufungua tawi katika Wilaya ya Wete na Mkoa wa Kaskazini Pemba. Uzinduzi huu umefanywa mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla aliyeambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Zanzibar, Naibu Waziri wa […]