Waliopita mchujo waitwa usaili BoT.

Benki Kuu ya Tanzania imetoa majina ya waliopita katika usaili wa maandishi huku ikiwaita katika usaili wa mahojiano na vitendo kwa baadhi ya kada. Tangazo hilo lililochapishwa katika tovuti ya BoT lilieleza wasailiwa waliopita katika mchujo huo wa awali wazingatie mambo kadhaa “Wasailiwa wote waliochaguliwa wanatakiwa kuzingatia muda na eneo la usaili na wanakumbushwa kufika […]

Umoja wa walimu wasio na ajira yataka umri wa kustaafu uwe miaka 50.

Umoja wa walimu wasio na ajira (Neto) wa kati ya mwaka 2015 – 2023 umewasilisha mambo 6 katika kikao cha mawaziri wawili, moja ya mambo hayo ni ikiwemo kupunguza umri wa kustaafu kwa walimu kutoka miaka 60 hadi 50 ili kutoa nafasi za ajira kwa vijana Serikalini. Mambo mengine yaliyowasilishwa ni pamoja na masuala ya […]

Hali ya Papa Francis yaleta matumaini.

Vatican imeeleza kuwa kiongozi wa kanisa la katoliki duniani, Papa Francis hayuko tena kwenye hatari ya kifo kutokana na maradhi yanayomsumbua. Imeelezwa kuwa dawa anazotumia Papa Francis zimeanza kuleta matokeo chanya kwenye mwili wake. Hali ya maendeleo ya kuimarika kwa afya ya kiongozi huyo imeonekana jana kwenye mfumo wa mapafu yake. Ni wiki tatu tangu […]

Serikali yakabidhi hospitali ya Mount Meru kifaa cha kisasa dhidi ya Saratani.

Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru jijini Arusha imepokea mashine ya kisasa ya mammografia itakayosaidia utambuzi wa saratani ya matiti ili kukokoa vifo vya wanawake wengi wanaofariki kwa ugonjwa huo. Mtaalamu wa Radiologia katika hospitali ya Mount Meru Dkt. Edward Joseph amesema “Utambuzi wa mapema ni hatua muhimu kwa mafanikio ya matibabu na kuongeza uwezekano […]

NMB yafuturisha watoto wenye uhitaji na wadau mbalimbali.

Benki ya NMB katika hali ya kudumisha upendo na mshikamano katika kipindi hichi cha Ramadhani ilifanikiwa kuandaa futari maalumu kwa watoto wenye uhitaji, wateja wao, viongozi wa dini na wadau mbalimbali katika ukumbi wa Superdome Masaki jijini Dar es Salaam. Lengo kuu la hafla hiyo ya NMB ilikuwa kutoa msaada wa vyakula na zawadi mbalimbali […]

BoT kushiriki maonyesho ya wiki ya wanawake

Benki Kuu ya Tanzania inashiriki katika maonyesho ya wiki ya wanawake yanayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijiji Arusha kuanzia tarehe 1 hadi tarehe 8 Machi 2025. Katika Maonyesho hayo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima alifanikiwa kutembelea banda la Benki Kuu na kupata elimu kuhusu masuala […]

Wizara ya Afya yasisitiza ARV kuendelea kutolewa bure.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV) zinapatikana bure kwa wagonjwa nchini Tanzania. Dk. Mollel ameyasema hayo wakati akishiriki katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya mradi wa Timiza Malengo uliofanyika Mkoani Lindi uliozinduliwa na Naibu Waziri wa ofisi ya Waziri […]

CRDB na FAO kuwasaidia wakulima wadogo.

Benki ya CRDB imeingia makubaliano na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo duniani (FAO) kwa lengo la kuwasaidia wakulima wadogo kufanya kilimo bora kupitia teknolojia za kisasa. Akizungumza katika halfa iliyofanyika makao makuu jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela amesisitiza utayari wa benki ya CRDB katika […]

Tanesco yatolea ufafanuzi taarifa ya kukosekana kwa umeme.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewatoa hofu wananchi kuwa maboresho yatakayofanyika kwanzia Februari 22-28 hayatafanyika kwa siku 6 mfululizo na hayatawaathiri wananchi kwa muda wote. Tanesco wametoa ufafanuzi kwa kusema “Tutakuwa na maboresho ya miundombinu yatakayofanyika katika kituo cha kupokea, kupoza na kusafirisha umeme cha Ubungo ambayo yanaweza kuathiri upatikanaji wa huduma ya umeme kwa […]

Mradi wa bwawa la Kidunda kumaliza tatizo la maji Dar-Es-Salaam.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Bw. Mkama Bwire amesema ujenzi wa mradi wa bwawa la Kidunda Mkoani Morogoro unatarajiwa kumaliza tatizo la maji Mkoa wa Dar-Es-Salaam. Mkama Bwire ameyasema hayo katika ziara ya jukwaa la wahariri (TEF) na waandishi wa habari kujionea maendeleo ya […]