Ajali ya ndege Philadelphia yaua 6 wakiwemo wagonjwa wawili.

Ajali ya ndege yatokea katika mji wa Philadelphia nchini Marekani ambapo ndege hiyo inaripotiwa kuanguka katika barabara karibu na jumba la maduka ya Rossevelt, hali iliyosababisha magari na nyumba zilizokuwa jirani kushika moto. Ndege hiyo inasemekana ilikuwa na watu 6 ambapo wawili wanadaiwa kuwa ni wagonjwa raia wa Mexico pamoja na wahudumua wanne , aidha […]

Rais Samia kuboresha maslahi ya walimu.

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itapitia upya maslahi kada ya ualimu nchini ili kuipa hadhi inayostahiki kada hiyo. Rais Samia ameyazungumza hayo Jijiji Dodoma wakati akizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2024. “Tutapitia upya maslahi ya kada ya ualimu nchini ili kuipa hadhi inayostahiki kada hii […]

Marekani yaitaka Rwanda kusitisha mapigano Congo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeitaka Rwanda kusitisha mapigano mara moja katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku ikitoa tahadhari juu ya kuunga mkono kundi la M23 lililoteka mji wa Goma. Katika mazungumzo na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Waziri Marco Rubio amesisitiza kuwa Marekani inasikitishwa sana na ongezeko la vurugu zinazoendelea mashariki […]

Rais Samia aongoza mkutano wa SADC-Organ

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) ameongoza mkutano wa dharura wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Asasi uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam. Katika Mkutano huo wa dharura, Rais Samia ameshiriki na Rais wa […]

M23 yateka uwanja wa ndege wa Goma.

Kundi la waasi wa M23 limeripotiwa kuudhibiti uwanja wa ndege wa Goma na kwa sasa upo mikononi mwao. Tukio hili limefanya kuzuia njia inayoleta misaada ya kibinadamu kutoka mataifa mbalimbali kuingizwa Congo. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa waasi hao wameteka uwanja wa ndege pamoja na wanajeshi zaidi ya 1200 wa Congo ambao wamejisalimisha na wameshikiliwa […]

CHADEMA yateuwa Katibu Mkuu na Wajumbe wapya wa kamati kuu

Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Tundu Lissu amemteua John Mnyika kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho akiwa katika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama. Mhe. Tundu Lissu pia ameteua Manaibu Katibu Wakuu wa Chama kama ifuatavyo Wakili Ally Ibrahim Juma kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar pamoja na Aman Golugwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara. Aidha amefanya […]

Trump kurudisha wazamiaji nchi walizotoka.

Baada ya kuapishwa kama Rais mpya wa Marekani, Donald Trump ameapa rasmi kulitumikia taifa hilo huku akisisitiza usalama wa mipaka, kukomesha uhamiaji haramu na kuwarudisha makwao wahamiaji haramu wote. Rais huyo wa 47 wa Marekani aliahidi hayo baada ya kuapishwa katika sherehe zilizofanyika katika ukumbi wa Capitol, Washington DC nchini Marekani. “Kwanza nitatangaza hali ya […]

Tanzania yathibitisha mtu mmoja apatikana na kirusi cha Marburg, Kagera.

Baada ya tetesi zilizoenea kuwepo kwa kirusi cha Marburg wiki kadhaa nyuma, imethibitishwa kuwa kirusi hicho kimepatikana kwa mtu mmoja tu baada ya sampuli zilizofanyiwa uchunguzi kukamilika. Hayo yamethibitishwa na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipotembelewa na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus akiwa Ikulu ya Chamwino, Jijini […]

Haaland kusalia Etihad mpaka 2034.

Mshambuliaji wa Manchester Erling Braut Haaland amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya ligi kuu nchini Uingereza. Haaland amesaini mkataba wa miaka 9 na nusu kuitumikia Manchester City. Mkataba huo unatarajiwa kumalizika mwaka 2034. Ingawa una kipengele cha kuununua ifikapo mwaka 2029 unaomruhusu kuweza kusajiliwa na timu nyingine endapo dau tajwa litafikiwa na […]

Chapo aapishwa kuwa Rais mpya Msumbiji.

Daniel Chapo wa Chama tawala cha FRELIMO ameapishwa kuwa Rais wa Msumbiji katika hafla iliyofanyika jijini Maputo. Rais Chapo ameahidi kuzingatia umoja na kuongoza juhudi za maendeleo kote nchini. Viongozi wa nchi mbalimbali walijumuika katika hafla hiyo akiwemo Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa aliyemuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.