Dkt Mpango ajiuzulu nafasi zake za utumishi wa umma.

Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Philip Mpango ameamua kujiuzulu kwa hiari kutoka kwenye nafasi zake za utumishi wa umma baada ya kuhudumu kwa miaka mingi katika nafasi mbalimbali za serikali. Dk Mpango ameshawahi kufanya kazi katika taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tume ya Mipango, na kama Waziri wa […]

Ofa ya Elon Musk kununua Chatgpt yapigwa chini.

Elon Musk amewasilisha ofa ya kununua OpenAI kampuni inayojulikana kwa kuunda ChatGPT kwa thamani ya dola bilioni 97.4 kwa Sam Altman ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa OpenAI na kusababisha mvutano kati ya hawa waanzilishi wawili wa kampuni. Musk na Altman walianzisha OpenAI mwaka 2015 kama shirika lisilo la kufaidika lakini hata hivyo uhusiano wao ulianza […]

Sam Nujoma wa Namibia afariki dunia.

Rais wa kwanza wa Namibia, Sam Nujoma amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95. Sam Nujoma aliongoza mapambano ya kupigania uhuru wa Namibia kutoka utawala wa Afrika Kusini mwaka 1990 ilipopata uhuru. Moja ya matukio yakukumbukwa kuhusu yeye ni mwaka 1960 alipokimbilia nchini Tanzania kutokana na vuguvugu lililotokea nchini Namibia ambapo Hayati Mwl. Nyerere […]

Duduzile Zuma afikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuchochea ghasia.

Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ajulikanaye kama Duduzile Zuma Sambudia amefikishwa mahakamani baada ya kushtakiwa kuchochea vurugu wakati wa ghasia za mwaka 2021 nchini Afrika Kusini ambapo zaidi ya watu 300 walipoteza maisha. Licha ya wakili wa binti Zuma amekana mashtaka hayo waendesha mashtaka wanadai kuwa Duduzile alichochea watu wengine kufanya […]

Mradi wa bwawa la Kidunda kumaliza tatizo la maji Dar-Es-Salaam.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Bw. Mkama Bwire amesema ujenzi wa mradi wa bwawa la Kidunda Mkoani Morogoro unatarajiwa kumaliza tatizo la maji Mkoa wa Dar-Es-Salaam. Mkama Bwire ameyasema hayo katika ziara ya jukwaa la wahariri (TEF) na waandishi wa habari kujionea maendeleo ya […]

Trump awagomea wanaume waliobadili jinsia kushiriki michezo ya wanawake.

Rais wa Marekani Donald Trump amesaini agizo linalopiga marufuku wanaume waliobadili jinsia kushiriki michezo ya wanawake ambapo amesema kuanzia sasa michezo ya wanawake itakuwa ya wanawake pekee. Trump ameyasema hayo akiwa Ikulu ya nchini Marekani akiwa amezungukwa na wanariadha wakike. Trump ametoa agizo hilo huku akitolea mifano wanaume wanaojidai kuwa wasichana kwa kuiba ushindi wa […]

Mwigulu Nchemba azindua Moduli ya kupokea rufaa Kieletroniki.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb.) amezindua rasmi matumizi ya Moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (NeST). Dkt. Mwigulu amezindua rasmi matumizi ya moduli hiyo Jijini Mwanza wakati wa mafunzo ya moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa (Complaint and […]

Agha Khan IV afariki dunia.

Kiongozi mkuu wa 49 wa Madhehebu ya Shia Ismailia na mwanzilishi wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), Mtukufu Aga Khan, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88 jijini Lisbon, Ureno. Mtukufu Aga Khan, anayefahamika kama Karim Al-Hussaini Aga Khan IV, alijulikana kwa mchango wake mkubwa katika kuboresha ustawi wa binadamu kupitia miradi […]

EAC na SADC kukutana kujadili amani ya DRC.

Uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unapanga kukutana kwenye mkutano wa kutafuta suluhisho la mgogoro mwa Mashariki mwa Congo. Kikao kinachotarajia kufanyika Jijini Dar es Salaam. Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye ni Rais wa Kenya Mhe. William Ruto ambapo amesema […]

Rais Trump kusitisha msaada Afrika Kusini.

Rais wa Marekani Donal Trump amesema kuwa atasitisha msaada Afrika Kusini mpaka pale uchunguzi utakapofanyika kujiridhisha kuhusu madai kwamba viongozi wa Afrika Kusini wanajenga matabaka kwenye umiliki wa ardhi kwa kuwapokonya wazungu ardhi za nchi hiyo ikionekana kama manyanyaso kwa watu weupe nchini Afrika Kusini. Trump ameyasema hayo kupitia akaunti yake mtandao wake wa Truth […]