Chato kumkumbuka Magufuli leo.

Ikiwa imepita miaka minne tangu Tanzania ipatwe na majonzi ya kumpoteza aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli Machi 17, 2021 kwa maradhi ya moyo leo taifa la Tanzania kwa ujumla litamkumbuka shujaa huyu. Ndugu, jamaa na marafiki watamkumbuka hayati John Pombe Magufuli kwa ibada itakayofanyika Chato ambayo imeandaliwa na familia yake. […]

Ada Tadea kuwapa kipaumbele wagombea wanawake wenye ulemavu

Chama cha African Democratic Alliance Party (Ada -Tadea) kimesema kuwa kitatoa fomu bure kwa wagombea wanawake na wenye ulemavu watakojitokeza kuwania nafasi ya Urais, ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu. Hayo yamezungumzwa na Katibu Mkuu wa Chama Bw. Salehe Msumari mjini Maswa Mkoani Simiyu wakati akiwapokea wanachama wapya 100 waliojiunga na Chama hicho kutoka vyama […]

Umoja wa walimu wasio na ajira yataka umri wa kustaafu uwe miaka 50.

Umoja wa walimu wasio na ajira (Neto) wa kati ya mwaka 2015 – 2023 umewasilisha mambo 6 katika kikao cha mawaziri wawili, moja ya mambo hayo ni ikiwemo kupunguza umri wa kustaafu kwa walimu kutoka miaka 60 hadi 50 ili kutoa nafasi za ajira kwa vijana Serikalini. Mambo mengine yaliyowasilishwa ni pamoja na masuala ya […]

Odinga akemea wanaotaka Rais Ruto atoke madarakani.

Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Rail Odinga amewajia juu wakosoaji wa Serikali ya Rais William Ruto wanaotaka aondoke madarakani huku akisema wanataka atoke aende wapi. Kauli hiyo imekuja baada ya siku chache nyuma Odinga kusaini makubaliano ya kufanya kazi na Rais William Ruto. Aidha katika mitandao ya kijamii baadhi ya Wakenya wamekuwa na kauli […]

LHRC yataka masheikh waachiwe huru kama hakuna ushahidi.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeiomba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwaachia Masheikh 51 wanaoshikiliwa katika magereza tofauti tofauti kwa takriban miaka 10 sasa bila kufikishwa mahakamani ikiwa ni kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977. LHRC inadai kuwa kitendo cha Jamhuri kuwafunga miaka yote hiyo bila kuwafikisha mahakamani […]

Rais wa zamani wa Ufilipino akamatwa kwa tuhuma za mauaji.

Aliyekuwa Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte, amekamatwa mjini Manila nchini Ufilipino kwa hati ya Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC). Duterte amekamatwa baada ya mahakama kutoa waranti inayomtuhumu kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu katika vita yake dhidi ya dawa za kulevya ambapo inaelezwa kuwa zaidi ya wafilipino elfu kumi waliuwawa. Duterte aliwekewa kizuizi […]

Hali ya Papa Francis yaleta matumaini.

Vatican imeeleza kuwa kiongozi wa kanisa la katoliki duniani, Papa Francis hayuko tena kwenye hatari ya kifo kutokana na maradhi yanayomsumbua. Imeelezwa kuwa dawa anazotumia Papa Francis zimeanza kuleta matokeo chanya kwenye mwili wake. Hali ya maendeleo ya kuimarika kwa afya ya kiongozi huyo imeonekana jana kwenye mfumo wa mapafu yake. Ni wiki tatu tangu […]

Serikali yakabidhi hospitali ya Mount Meru kifaa cha kisasa dhidi ya Saratani.

Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru jijini Arusha imepokea mashine ya kisasa ya mammografia itakayosaidia utambuzi wa saratani ya matiti ili kukokoa vifo vya wanawake wengi wanaofariki kwa ugonjwa huo. Mtaalamu wa Radiologia katika hospitali ya Mount Meru Dkt. Edward Joseph amesema “Utambuzi wa mapema ni hatua muhimu kwa mafanikio ya matibabu na kuongeza uwezekano […]

NMB yafuturisha watoto wenye uhitaji na wadau mbalimbali.

Benki ya NMB katika hali ya kudumisha upendo na mshikamano katika kipindi hichi cha Ramadhani ilifanikiwa kuandaa futari maalumu kwa watoto wenye uhitaji, wateja wao, viongozi wa dini na wadau mbalimbali katika ukumbi wa Superdome Masaki jijini Dar es Salaam. Lengo kuu la hafla hiyo ya NMB ilikuwa kutoa msaada wa vyakula na zawadi mbalimbali […]

TRA yakemea wanaodanganya watu kufuta madeni ya kodi.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda amekemea vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na watu wanaodai kuwa na uwezo wa kusamehe madeni ya kodi. Mwenda ametoa onyo hilo baada ya jeshi la polisi kukamata watuhumiwa wawili wanaodaiwa kufanya udanganyifu kuwa wao ni maofisa wa TRA na kuwa wanauwezo wakusamehe madeni ya kodi. Mwendo […]