BoT yahimiza wananchi kuacha kutumia Fedha za kigeni kununua bidhaa nchini.

Benki Kuu imewataka wananchi wote kutumia Shilingi ya Tanzania wakati wanapofanya miamala yao nchini katika nyanja mbalimbali. Hayo yamezungumzwa na Gavana wa Benki Kuu Tanzania Bw. Emmanuel Tutuba ambaye amesema ni kosa kununua, kuuza bidhaa na huduma hapa nchini kwa kutumia fedha za kigeni. Ameongeza kuwa kutumia fedha za kigeni ni kuhujumu uchumi wetu na […]