Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) limeiomba Mamlaka ya Udhibiti na Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kibali cha ujenzi wa njia ya kusambaza gesi asilia yenye urefu wa mita 300 kutoka bomba la usambazaji wa gesi asilia lililopo Tegeta hadi eneo la mradi wa kujenga kituo cha kushindilia gesi asilia cha PUMA Energy Tanga Limited kilichopo Tegeta Manispaa ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam