Super Cup kuipa dunia El Classico

El Classico mechi pendwa katika mpira wa miguu itawakutanisha mahasimu wakubwa wa mpira nchini Hispania katika siku ya Jumapili ya Januari 12, mwaka 2025.

Barcelona waliofuzu fainali hiyo kwa kumfunga Athletic Bilbao 2-0 watavaana na Real Madrid waliofuzu kwa kuiondoa Real Mallorca kwa mabao 3-0.

Mchezo huo unaleta kumbukumbu nyingi ikiwa mara ya mwisho wawili hao kukutana kwenye fainali hiyo ya Super Cup Real Madrid waliweza kunyakua ubingwa huo kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Barcelona.

Kwa upande wa Barcelona watakuwa na nafasi ya kubeba kombe lao la kwanza msimu huu chini ya kocha mpya Hans Flick. Mara ya mwisho wawili hao wamekutana kwenye mchezo wa ligi ya La Liga msimu huu huku Barcelona wakiibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *