Simbachawene atangaza usaili wa walioomba ajira za ualimu kufanyika

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema kuwa usaili wa walioomba ajira kwenye kada ya ualimu utafanyika kuanzia Januari 14 hadi Februari 24 kwenye vituo vya usaili vilivyopo kwenye Mikoa wanaoishi wasailiwa.

Mhe. Waziri ameyazungumza haya kwa waandishi wa habari akiwa kwenye ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba Jijini Dodoma.

“Nafasi zilizotangazwa kujazwa kwenye kada ya ualimu zilikuwa ni 14,648 tu lakini mpaka sasa walioomba ajira kupitia Ajira Portal ni watu 201,707 utaona idadi ilivyo kubwa ya watu wanaohitaji kujaza nafasi hii lakini uhitaji wetu kwa sasa ni huo” alisema Simbachawene.

Aidha Waziri amesema kuwa kada hiyo hapo awali walikuwa wakipangwa moja kwa moja kwenye vituo vya kazi baada ya kupata ajira lakini sasa ni lazima wasailiwe ili wapate wenye sifa zinazohitajika kabla ya kupangiwa vituo vya kazi.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *