Shule na Vyuo kufungwa Dar es Salaam kupisha mkutano wa kimataifa wa Nishati

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza kuwa shule zote za msingi, sekondari, na vyuo vya elimu jijini Dar es Salaam zitafungwa kwa muda wa siku mbili, Januari 27 na Januari 28, 2025.

Katika taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa, alisema, “Tangazo hili linahusu shule na vyuo vya serikali na binafsi. Wadau wote wa elimu wanahimizwa kutii agizo hili ili kuepuka changamoto za usafiri zitakazotokana na kufungwa kwa baadhi ya barabara.

Masomo yataendelea kama kawaida Januari 29, 2025.”Hatua hii inalenga kuzuia usumbufu unaoweza kusababishwa na kufungwa kwa barabara kutokana na ujio wa wageni wengi wanaohudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, ambao utafanyika jijini Dar es Salaam kesho na keshokutwa.

Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania, Benki ya Dunia, na Benki ya Maendeleo ya Afrika.Mkutano huo utahudhuriwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan; marais 24 wa Afrika; wawakilishi wa wakuu wa nchi na serikali 21 za Afrika; wakuu wa taasisi sita za kimataifa, akiwemo Rais wa Benki ya Dunia, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, na Rais wa Taasisi ya Rockefeller; pamoja na washirika wa maendeleo watano.Jumla ya washiriki 2,600 kutoka ndani na nje ya Tanzania wamesajiliwa kushiriki katika mkutano huo.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *