Serikali yatangaza kumalizika kwa mlipuko wa Marburg

Serikali yatangaza kumalizika kwa mlipuko wa Marburg baada ya siku 42 za ufuatiliaji bila kesi mpyaWakati huohuo, Zanzibar imeeleza hatua inazochukua kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa Mpox, ambao ulitangazwa kuwepo Tanzania siku ya Jumatatu.

Mlipuko wa pili wa ugonjwa huo ulithibitishwa Januari mwaka huu baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza kuwa watu wanane walifariki kutokana na ugonjwa huo unaoshukiwa.

Hata hivyo, Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, alitangaza Jumatatu, Machi 13, 2025, kuwa watu wawili walipoteza maisha wakiwa kwenye matibabu.

Ugonjwa huo uliripotiwa katika wilaya ya Biharamulo, mkoa wa Kagera, kaskazini magharibi mwa Tanzania, eneo linalopakana na Uganda upande wa kaskazini na Rwanda upande wa magharibi.Bi Mhagama alisema kuwa Tanzania sasa imekamilisha kipindi cha siku 42 za ufuatiliaji bila kuripotiwa kesi mpya, hivyo kuruhusu kutangazwa rasmi kumalizika kwa mlipuko huo.

Kesi ya mwisho ya MVD ilithibitishwa Januari 28, 2025. Kufikia Machi 11, 2025, tumetimiza siku arobaini na mbili (42) tangu kuthibitishwa kwa kesi ya mwisho,” alisema katika taarifa yake.”Kitaalamu, tunakidhi vigezo vya kutangaza kumalizika kwa mlipuko wa MVD. Hivyo basi, leo Machi 13, 2025, natangaza rasmi kuwa mlipuko wa MVD nchini umefikia kikomo,” aliongeza.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *