Samia Women super Cup kupigwa Arusha leo machi 4.

Kombe la Samia Women Super Cup 2025 linatarajiwa kuanza leo, Machi 4, 2025, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.Mashindano haya ya kwanza kabisa yanashirikisha timu nne bora kutoka Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania msimu wa 2024/2025, Fountain Gate Princess, JKT Queens, Simba Queens, na Yanga Princess.

Ratiba ya Mashindano leo Machi 4, 2025: Mechi za nusu fainali ili kupata timu zitakazocheza fainali.Machi 6, 2025 kutakua na Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu na fainali kuu.Mashindano haya yanafanyika sambamba na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake, ambayo mwaka huu yataadhimishwa kitaifa mkoani Arusha.

Hii inafanya Kombe la Samia Women Super Cup kuwa jukwaa muhimu la kuonesha mchango wa wanawake katika michezo na kukuza usawa wa kijinsia kupitia mpira wa miguu.Timu zote shiriki zilifika Arusha tarehe 2 Machi 2025 kwa maandalizi ya mashindano haya. Mashabiki wanatarajia mechi kali, huku matukio na matokeo yakitarajiwa kusambazwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania imesimama kwa muda ili kutoa nafasi kwa Samia Women Super Cup, jambo linaloonesha umuhimu wa mashindano haya katika ratiba ya michezo nchini.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *