Real Madrid tayari wamekamilisha usajili wa Trent Alexander-Arnold.Kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania, Madrid wamehititimisha makubaliano ya pande zote mbili kuhusu kumsajili Alexander-Arnold kama mchezaji huru kuelekea Santiago Bernabéu.
Ripoti hiyo pia inadai kuwa, kwa mazingatio ya heshima kwa Liverpool, Madrid hawata fanya utambulisho rasmi wa uhamisho huo kipindi msimu unaendelea, hasa kwa kuwa kuna uwezekano wa timu hizo kukutana katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.
Zaidi ya hayo, Madrid wanatarajia kupata msaada kutoka kwa Liverpool kuelekea kombe la dunia la vilabu.
Mkataba wa Alexander-Arnold na vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza unamalizika Juni 30, lakini Madrid wanatumai juu ya uwezekano wa Liverpool kuwaruhusu beki huyo wa kulia kuchezea klabu hiyo katika Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA 2025 litakalo fanyika mwezi juni hadi julai huko nchini Marekani.