Klabu ya Aston Villa inatarajiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford kabla ya dirisha la usajili kufungwa siku ya Jumatatu.
Marcus Rashford atajiunga na Aston Villa kwa mkopo wa wa msimu mzima huku klabu ya Aston Villa ikihusika kulipa mshahara wake.
Rashford amekubali kujiunga na Aston Villa baada ya maongezi na kocha wa Aston Villa Unai Emery aliyemhakikishia atakuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Aston Villa kinachoshirikia ligi ya mabingwa barani Ulaya.