Rais wa zamani wa Ufilipino akamatwa kwa tuhuma za mauaji.

Aliyekuwa Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte, amekamatwa mjini Manila nchini Ufilipino kwa hati ya Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC).

Duterte amekamatwa baada ya mahakama kutoa waranti inayomtuhumu kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu katika vita yake dhidi ya dawa za kulevya ambapo inaelezwa kuwa zaidi ya wafilipino elfu kumi waliuwawa.

Duterte aliwekewa kizuizi katika uwanja wa ndege wa Manila baada ya kurejea kutoka safari ya Hong Kong kulingana na Serikali ya Ufilipino.

Wakili wake Bw. Salvador Panelo amedai kuwa kukamatwa kwa Duterte ni kinyume cha Sheria kwasababu Ufilipino ilijiondoa katika mahakama ya ICC wakati Duterte akiwa Rais.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *