Rais wa FIFA Gianni Infantino Afungua milango ushiriki wa Urusi katika soka

Mashindano ya 23 ya Kombe la Dunia yatafanyika Amerika Kaskazini, ambapo Marekani, Canada, na Mexico zitakuwa wenyeji wa mashindano hayo kwa mara ya kwanza kwa mfumo ulioongezeka wa timu 48. Mataifa hayo yalishinda zabuni dhidi ya Morocco kupata haki ya kuwa wenyeji.

Hii pia itakuwa mara ya kwanza katika historia kwa mataifa matatu kushiriki jukumu la kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia, ambapo mechi zitachezwa katika viwanja 11 nchini Marekani, miji mitatu nchini Mexico, na miji miwili nchini Canada.

Mataifa haya matatu yamefuzu moja kwa moja kwenye mashindano hayo, huku timu zingine 45 zikihitajika kupita hatua za kufuzu. Droo ya makundi ya mashindano haya hapo baadae Desemba 2025.

Hata hivyo, Rais wa FIFA, Gianni Infantino, amesema yuko tayari kuzingatia uwezekano wa kurudi kwa Urusi kwenye mashindano hayo.

Baada ya Urusi kuingia katika mgogoro wa uvamizi nchini Ukraine mnamo Februari 2022, Shirikisho la Soka la Urusi (RFU) lilifungiwa kushiriki mashindano yote ya FIFA na UEFA.

Kutokana na mgogoro unaoendelea, Urusi ilikuwa taifa pekee la UEFA ambalo halikushiriki droo ya kufuzu kwa Kombe la Dunia. Lakini, kutokana na ushirikiano wa kisiasa kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump, na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ambao wamekuwa wakijadili makubaliano ya amani, Infantino anafikiria uwezekano wa kubadilisha msimamo kuhusu Urusi kushiriki mashindano chini ya shirikisho la mpira wa miguu duniani.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *