Rais wa Marekani Donal Trump amesema kuwa atasitisha msaada Afrika Kusini mpaka pale uchunguzi utakapofanyika kujiridhisha kuhusu madai kwamba viongozi wa Afrika Kusini wanajenga matabaka kwenye umiliki wa ardhi kwa kuwapokonya wazungu ardhi za nchi hiyo ikionekana kama manyanyaso kwa watu weupe nchini Afrika Kusini.
Trump ameyasema hayo kupitia akaunti yake mtandao wake wa Truth kisha baadae akalizungumzia hadharani mbele ya waandishi wa habari.
Kauli hizi za Trump zimekuja baada ya wiki kadhaa nyuma rafiki yake na bilionea Elon Musk ambaye pia ni raia wa Afrika Kusini kulalamika watu weupe wananyanyaswa Afrika Kusini.