Rais Samia kuboresha maslahi ya walimu.

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itapitia upya maslahi kada ya ualimu nchini ili kuipa hadhi inayostahiki kada hiyo.

Rais Samia ameyazungumza hayo Jijiji Dodoma wakati akizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2024.

“Tutapitia upya maslahi ya kada ya ualimu nchini ili kuipa hadhi inayostahiki kada hii kama mama wa taaluma zote duniani”

Rais aliendelea kwa kusema “Sera hii inamaanisha upanuzi wa miundombinu ya elimu nchini hivyo niitake TAMISEMI iandae mkakati wa kutekeleza Sera hii kwa ujenzi wa miundombinu nchini, mafanikio ya Sera hii yatategemea utekelezaji hivyo kila mmoja atekeleze wajibu wake, watoto wahudhurie masomo, wazazi wahakikishe watoto wanafuatilia masomo na Serikali tusimamie ubora wa elimu na kuinua hadhi ya Mwalimu nchini,”.

Aidha Rais Samia amesisitiza kuwa utekelezaji wa sera hii unahitaji fedha nyingi huku akisisitiza ukusanyaji wa mapato ndani ya nchi uongezeke kupitia kulipa kodi na kuwahimiza wanaonunua bidhaa kudai risiti na wanaouza kutoa risiti ili kukomesha wanaokwepa kulipa kodi.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *