Rais Samia aongoza mkutano wa SADC-Organ

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) ameongoza mkutano wa dharura wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Asasi uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Katika Mkutano huo wa dharura, Rais Samia ameshiriki na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema pamoja na Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera.

Aidha Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi wameshiriki kwa njia ya mtandao.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *