Puma msambazaji rasmi wa mipira ligi kuu Uingereza msimu ujao

Puma imeteuliwa kuwa msambazaji rasmi wa mipira ya Ligi Kuu ya England kuanzia msimu wa 2025/26, hatua inayomaliza utawala wa Nike wa miaka 25 kwenye ligi hiyo.

Mabadiliko haya makubwa yanakuja baada ya mazungumzo ya kuongeza mkataba wa Nike kushindikana, kama ilivyoripotiwa na The Athletic mwaka 2023.

Kwa sasa, Puma tayari ni msambazaji wa mipira kwa ligi kubwa za Ulaya kama Serie A na La Liga.

Kupitia dili hili jipya, kampuni hiyo inalenga kuimarisha zaidi uwepo wake katika soko la soka, huku ripoti za Sky Sports zikibainisha kuwa mkataba huu ni wa thamani kubwa zaidi kuliko ule wa Nike, ambao ulikuwa na thamani ya pauni milioni 10 kwa mwaka.

Hatua hii ni sehemu ya mkakati mpana wa Puma wa kuinua hadhi yake katika sekta ya michezo.

Mbali na kushirikiana na vilabu vikubwa kama Manchester City, Puma pia inadhamini wachezaji nyota kama Kai Havertz, huku ikiendelea kuboresha ubunifu wake katika vifaa vya soka.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *