Elon Musk amewasilisha ofa ya kununua OpenAI kampuni inayojulikana kwa kuunda ChatGPT kwa thamani ya dola bilioni 97.4 kwa Sam Altman ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa OpenAI na kusababisha mvutano kati ya hawa waanzilishi wawili wa kampuni.
Musk na Altman walianzisha OpenAI mwaka 2015 kama shirika lisilo la kufaidika lakini hata hivyo uhusiano wao ulianza kupungua baada ya Musk kuachana na kampuni hiyo mwaka 2018.
Kwa sasa OpenAI imekuwa na mafanikio makubwa kibiashara ikiwa na teknolojia ya akili mnemba (AI) inayotumika sana kote duniani.
Altman alijibu ofa hiyo kwa kutumia mtandao wa X akisema “Hapana asante lakini kama unapenda tutanunua X kwa dola bilioni 9.74.”
OpenAI kupitia CHATGPT ina sifa kubwa kwa kuleta maendeleo katika sekta ya AI, ikiwa imesaidia watu wengi kwa madhumuni mbalimbali, kama vile kujifunza, kufanya kazi, na kujibu maswali