Nyota raia wa ufaransa Phillipe Mateta akutana na ajali mbaya katika mchezo wa FA

Nyota wa Crystal Palace Mateta apata majeraha katika harakati za kuwania mpira ana kwa ana na kipa Roberts wa millwall alietoka nje ya boksi lake na kufanya madhambi yaliyo gharimu hali ya kiafya ya mpinzani wake.

Ajali hio ilio husisha maeneo ya kichwani mwa mateta mshambuliaji wa Crystal Palace ili mfanya kipa Roberts kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya mwamuzi Michael Oliver kukagua tukio hilo kwenye picha za marudio ya VAR pembeni ya uwanja.

Madaktari tisa walifika mahala pa tukio kumtibia Mateta – ambaye alikuwa amelazwa kwenye nyasi kwa dakika nane.

Mchezaji huyo wa Kifaransa kisha aliinuliwa kwenye kitanda cha huduma huku akipatiwa oksijeni – na mara moja akapelekwa hospitalini kwa gari la wagonjwa lililokuwa pembeni ya uwanja.

Mateta aliandika kwenye Instagram yake masaa machache baada ya mchezo kwa ujumbe uliosomeka “Asante kwa ujumbe wenu wa fadhili. Niko sawa. Natumaini kurudi hivi karibuni. Na nguvu zaidi kuliko wakati wote. Hongera kwa kazi nzuri leo. Ninawapenda.”

Baada ya Crystal Palace kufanikiwa kufika robo fainali kwa ushindi wa 3-1, kocha Oliver Glasner alifichua kuwa Mateta anapatiwa matibabu kwa jeraha kubwa la sikio.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *