Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Darwin Nunez anatarajiwa kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu ikiwa ametimiza misimu mitatu tangu alipojiunga na majogoo wa Anfield mwaka 2022.
Nunez ameshindwa kufikia matarajio ya wengi tangu alipofika Liverpool akitokea Benfica, jambo ambalo limefanya Liverpool wafikirie kumuuza mshambuliaji huyo.
Aidha Nunez alitarajiwa kujiunga na Al Nassr ya Saudi Arabia dirisha la Januari lakini Liverpool hawakuwa tayari kumuuza kwa wakati huo ila maneno ya hivi karibuni ya kocha Arne Slott yameonyesha wazi mshambuliaji huyo ataondoka Liverpool.
Slott amekaririwa akisem hafurahishwi na mwenendo wa mshambuliaji huyo na kama ni nafasi ameshampatia za kutosha lakini bado hajashawishika naye.