NMB yafuturisha watoto wenye uhitaji na wadau mbalimbali.

Benki ya NMB katika hali ya kudumisha upendo na mshikamano katika kipindi hichi cha Ramadhani ilifanikiwa kuandaa futari maalumu kwa watoto wenye uhitaji, wateja wao, viongozi wa dini na wadau mbalimbali katika ukumbi wa Superdome Masaki jijini Dar es Salaam.

Lengo kuu la hafla hiyo ya NMB ilikuwa kutoa msaada wa vyakula na zawadi mbalimbali kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. Zawadi ambazo zilikabidhiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

Aidha Waziri Mkuu ameipongeza benki ya NMB na kusisitiza kuwa Serikali inatambua changamoto zinazowakabili watoto yatima na hatua ya msaada wa NMB kwa watu wenye uhitaji inapaswa kuwa mfano kwa taasisi nyingine.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB, CPA David Nchimbi amemshukuru Waziri Mkuu na wageni waalikwa kwa kushiriki katika hafla hiyo akielezea kuwa Ramadhani ni fursa ya kutafakari huruma, ukarimu na mshikamano ndani ya jamii.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *