Benki ya NMB sasa inapatikana Mikoa yote Zanzibar. Hii ni baada ya kufungua tawi katika Wilaya ya Wete na Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Uzinduzi huu umefanywa mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla aliyeambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Zanzibar, Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Hamad Hassan Chande pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Dhamira kuu ikiwa kuendeleza ujumuishwaji wa kifedha nchini (financial inclusion). Uzinduzi wa tawi hili unakwenda kuchochea upatikanaji wa huduma za kifedha kwa urahisi na kwa gharama nafuu.
Kupitimia dhima ya uwajibikaji kwa jamii (CSI) NMB imekabidhi vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 110. Vifaa hivyo ni pamoja na vitanda vya hospitalini 10, vitanda vya kujifungulia 5, mashuka 80 na vifaa mbalimbali.