Nyota wa zamani wa Barcelona, Psg na timu ya taifa ya Brazil Neymar Junior rasmi amerejea katika klabu yake ya zamani ya Santos ya nchini Brazil. Neymar amefanya hivyo baada ya Al Hilal kusitisha mkataba wake.
Neymar ambaye amekuwa na wimbi la majeruhi katika maisha yake ya soka alishindwa kutamba na Al Hilal ya Saudi Arabia baada ya mfululizo wa majeraha jambo ambalo limefanya klabu hiyo kusitisha huduma na yeye.
Rasmi Neymar amerejea nyumbani Santos klabu iliyomkuza kabla ya kutimkia Fc Barcelona. Neymar atakumbukwa kuwa na mchango mkubwa kwenye soka la ulaya hususan kwenye kipaji chake ambacho kilionekana ni burudani tosha kwa wengi.