Fainali ya kombe la Carabao imeshuhudia Newcastle United ikiibuka bingwa wa kombe hilo baada ya kuichapa Liverpool 2-1 fainali iliyofanyika katika uwanja wa Wembley.
Ubingwa huo umekuwa wa kihistoria kwa Newcastle ambao wameshinda taji hilo baada ya ukame wa miaka 70 bila kombe lolote la ndani huku mara ya mwisho kubeba taji ikiwa mwaka 1959.
Eddie Howe anaingia kwenye historia ya timu hiyo kama kocha aliyekata ukame wa makombe kwa klabu hiyo ambayo imepitia wachezaji mashuhuri kibao akiwemo Allan Shearer kinara wa mabao wa muda wote katika ligi kuu nchini Uingereza.