Mwigulu Nchemba azindua Moduli ya kupokea rufaa Kieletroniki.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb.) amezindua rasmi matumizi ya Moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (NeST).

Dkt. Mwigulu amezindua rasmi matumizi ya moduli hiyo Jijini Mwanza wakati wa mafunzo ya moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa (Complaint and Appeal Management Module) katika Mfumo wa NeST.

Katika Hotuba yake iliyosomwa na Kamishna wa Sera ya Ununuzi wa Umma, Dkt. Frederick Mwakibinga ilinukuliwa kwa kusema

“Moduli hii mpya inalenga kurahisisha zoezi zima la uwasilishaji wa malalamiko na rufaa kwa upande wa wazabuni na pia itawezesha taasisi nunuzi na Mamlaka ya Rufani kushughulikia Malalamiko na rufaa kupitia Moduli hii hivyo kupunguza muda na gharama zinazo ambatana na zoezi zima la utoaji wa haki,” amesema Dkt. Mwigulu.

Mafunzo ya matumizi rasmi ya moduli awamu ya pili kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa yametanguliwa na mafunzo ya awamu ya kwanza yaliyofanyika Mwezi Mei 2024 kwa mikoa ya kanda ya Pwani iliyojumuisha Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Morogoro.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *