Mmiliki wa Manchester United kushirikiana na Tanzania maendeleo ya wanyamapori na utalii

Mmiliki mwenza wa Manchester United, Sir Jim Ratcliffe, ameahidi kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kukuza uhifadhi wa wanyamapori na maendeleo ya utalii.

Ratcliffe, ambaye pia ni mwenyekiti wa kampuni ya mafuta na gesi ya INEOS, alitoa ahadi hiyo wakati wa mkutano wake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, katika ofisi yake mjini Monaco, Ufaransa.

Wakati wa mkutano huo, Ratcliffe alisifu juhudi za Tanzania katika kulinda rasilimali za wanyamapori na kukuza utalii, akisema kuwa nchi hiyo ni miongoni mwa maeneo machache duniani yenye idadi kubwa ya wanyama wakubwa wa porini.

“Ninatembelea Tanzania mara kwa mara, na nitarejea tena mwaka huu. Ninapanga kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan ili kumsifu kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuhifadhi urithi wa asili wa nchi.

Tanzania imehifadhi wanyamapori wake kwa kiwango cha kipekee kisicho na mfano mahali pengine popote,” alisema Ratcliffe.

Kwa upande wake, Dkt. Abbasi alitoa ujumbe maalum kutoka kwa serikali ya Tanzania, akimhimiza Ratcliffe kutumia ushawishi wake kupitia vilabu vyake vya michezo kusaidia juhudi za Rais Hassan za kuitangaza Tanzania kimataifa.

Ratcliffe aliahidi kutekeleza ombi hilo na kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala ya uhifadhi na utalii, akisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha urithi wa asili wa nchi unalindwa kwa vizazi vijavyo.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *