Mkuu wa polisi Chanika SP awadhi chico afariki kwa ajali ya Gari

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chanika SP Awadhi Mohamed Chico amefariki dunia siku ya leo saa moja asubuhi kwa ajali ya gari katika barabara ya Pugu wakati akielekea kazini.

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imethibitisha ajali iliyotokea leo Machi 17, mwaka huu, saa moja asubuhi, barabara ya Nyerere, eneo la Pugu, Mwisho wa Lami na kusababisha kifo cha Mkuu wa Kituo cha Polisi Chanika, Awadhi Chico.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Faustine Mafwele, akizungumza na wanahabari leo, amesema ajali hiyo imetokea baada ya dereva wa daladala yenye namba za usajili T 580 EAE, aina ya Tata inayofanya safari zake kati Zingiziwa Chanika na Machinga Complex Ilala akitokea Pugu kwenda Gongo la Mboto.

Amesema gari hilo liligongana na gari namba T 952 AMD aina ya Toyota Prado, iliyokuwa ikiendeshwa na PF 15950 SP Awadh Mohamed Chico, ambaye ni mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chanika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala ACP Yustino Mgonja amethibitisha tukio hilo akitangaza kifo cha SP Awadhi muda mfupi uliopita kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za Jeshi la Polisi Tanzania.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali kuu ya Polisi Baracks na kesho tarehe 18/03/2025 utaagwa hospitalini hapo na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu Dar es Salaam.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *