Chama cha waamuzi nchini Uingereza kimesema kuwa kinasimama na maamuzi ya mwamuzi Michael Oliver baada ya sakata lake la kadi nyekundu aliyotoa ya beki wa Arsenal Myles Lewis Skelly kwenye mchezo wa Arsenal dhidi ya Wolves. Chama hicho kimesema kuwa wanaona ni kadi sahihi licha ya watu mbalimbali kupinga.

Michael Oliver yupo chini ya uangalizi mkali baada ya yeye na familia yake kutishiwa maisha na mashabiki wa Arsenal huku wengi wakisema hawataki achezeshe tena mechi za klabu hiyo.

Arsenal imekuwa na bahati mbaya linapokuja swala la maamuzi ya marefa na mara kibao wamekuwa wakiangusha alama muhimu swala ambalo limefanya mashabiki wake wengi kuamini kuwa waamuzi wanatumika kuiangusha timu hiyo.

Katika kipindi chake cha mechi alizowahi kuchezesha, Michael Oliver ameipa Arsenal kadi nyekundu nyingi kuliko timu yoyote ile (8) kitu ambacho kinaonekana kama chuki binafsi kwa washika bunduki wa London.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *